Figo zenye afya kwa wote- huduma bora za figo kwa kupunguza tofauti ya ujuzi

Mtu mzima 1 kati ya 10 duniani kote wanao, na husababisha vifo endapo huachwa bila tiba.
Vifo vitokanavyo na magonjwa hayo huongezeka kila mwaka, na hutabiriwa itakuwa ya 5 katika sababu ya vifo ifikapo mwaka 2040.
Tafauti ya kiujuzi ni kikwazo kwenye vita dhidi ya magonjwa ya figo, pamoja na ongezeko la vifo linaambatana nayo.

Kumekuwa na tofauti ya elimui juu ya magonjwa ya figo, inayozidi kubainika na kukua kwenye ngazi zote za utoaji huduma za afya:

Jamii

Ukinzani wa kuwa na elimu na uelewa mzuri juu ya afya ya figo huchangiwa na ugumu na utata wa taarifa zenyewe, muamko hafifu, udhaifu kwenye uelewa wa elimu ya msingi ya afya, ufinyu wa taarifa za magongwa ya figo na ukosekanaji wa utayari wa kijifunza.

Read more

Watumishi wa afya

Kihunzi kingine cha kukivuka ili kuongeza muamko ni kuongeza elimu yenye dira kwa matabibu ambao ndio waaangalizi wa wagonjwa.

Read more

Watunzi wa sera za afya

Pamoja na kuwa magonjwa ya figo ni changamoto kubwa ya kiafya kwenye jamii na duniani,bado sio kipaumbele kwenye ajenda za kiafya za serikali (WKD 2008), na msukumo wa kisiasa kuelekezwa magonjwa kuu manne yasioambukiza-magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, saratani, kisukari na magonjwa sugu ya mapafu.

Read more

kamati kuu ya siku ya figo duniani (WKD) inawataka walimwengu wote sio tuu kuwa na muamko wa magonjwa ya figo, bali hata kujua vipimo vyao vya figo vikoje! Mfano, kujua shinikizo yake la damu lipo ngapi na malengo ya lifike ngapi. Haya ni malengo ya wote kwa jumuiya ya mambo ya figo ulimwenguni- madaktari, wanasayansi, wauguzi, wahudumu wengine wa afya, wagonjwa, watawala, wataalam wa sera, watumishi wa kiserikali na jumuiya za mambo ya figo. Wote huhitajika kujua namna za kuongeza muamko na kipaumbele juu ya mambo ya figo kwenye ngazi za kisera na ambayo zitaleta manufaa kwa wagonjwa wa figo na nafuu za kibajeti kwenye sekta ya afya.

Zaidi, tunawataka wana jamii kufuata kanuni bora za afya kwenye lishe na mwenendo wa maisha (kufanya mazoezi, unywaji wa maji safi na salama, lishe bora, udhibiti wa matumizi ya tumbaku na udhiniti wa mabadiliko ya tabia-nchi) kwa lengo la kudumisha afya njema ya figo na ufanyajikazi wake kwa wagonjwa wa figo na kuongeza muamkowa umuhimu wa figo kwa ujumla wake.

Tunataka ongezeko la kuoaji elimu kwa wagonjwa wa figo (ikiwemo mambo ya lishe bora na mwenendo wa maisha)ili kuwajengea uwezo wagonjwa, wasaidizi wa wagonjwa na wengineo kufikia malengo muhimu ya kiafya na yakimaisha yenye kuleta maana kwa wagonjwa wa figo.

Tunawatia moyo na kuungana na wahudumu wa afya za msingi kwenye kuboresha utambuzi na utabibu wa magonjwa ya figo na kwenye kushughulikia wigo mzima wa mambo ya figo, kuanzia ngazi zote za kinga hadi huduma kwa figo zilizofeli kabisa.

Tunatoa wito wa kuzijumuisha programu za tiba na kinga za magonjwa ya figo kwenye programu kuu jumuishi za huduma na kinga ya magonjwa yasioambukiza ambazo ni muhimu kwenye maswala ya utambuzi wa mapema na ufwatiliajiaji wa huduma za figo kitaifa, na maswala muambata kama sonona, msongo, utegemezi na udhaifu wa kimwili. Pia ,kuongeza elimu na mbinu za tiba ambazo hulenga kupunguza dalili na madhara ili wagonjwa na wasaidizi wao wabaki na maisha bora kiafya.

lazima kuwahusisha viongozi na wanasiasa, kielimu na kihamasa, juu ya madhara yatokanayo na magonjwa ya figo na figo kufeli na namna ambayo huongeza mzigo kwa mwananchi waliopo chini yao na kwa mfumo mzima wa utoaji afya. Hili litawahamasisha viongozi hao kupitisha maswala ya kibajeti na kisera yanayohusu afya ya figo ili kupunguza ukubwa wa tatizo duniani na kuboresha maisha ya wagonjwa wa figo.

Jihusishe

Pakua taarifa zetu kwenye tovuti

Mahitaji ya kampeni ya mwaka 2022

Picha kwa ajili ya kampeni ya mwaka 2022

Nembo ya WKD

Hakimili na ruhusa ya matumizi

Rasilimali za ziada

Vifurushi vya mashuleni

Taarifa kwa vyombo vya habari

Ongezea matukio

Duniani kote, watu huadhimisha kwa pamoja siku ya figo duniani namo tarehe 10 Machi, 2022. utaiadhimishaje? Tujulishe kwa kuposti taarifa zako kwenye ramani ya matukio hapo juu!

Sambaza ujumbe wetu

Tunakuhitaji wewe kutusaidia kuongeza muamko na kuwawezesha watu wanaoishi na magonjwa ya figo!

Jifunze zaidi kuhusu siku ya figo duniani WKD

Siku ya figo duniani (WKD)

Kampeni ya kidunia kuongeza muamko wa umuhimu wa figo zetu

Siku ya figo duniani hujirudia kila mwaka. Mamia ya matukio huambata na maadhimisho yakiwemo vipimo vya afya kwa umma nchini Argentina na hata mbio ndefu za marathoni nchini Malaysia. Vyote hufanyika kuongeza muamko. Muamko na elimu juu ya jinsi ya kujikinga, visababishi vya magonjwa ya figo na namna bora kuishi na ugonjwa wa figo. Tunatamani afya njema ya figo kwa watu wote!

Unaweza fanya nini kwa afya ya figo zako?

Kuna njia kadhaa za kukinga na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya figo.Tazama kanuni 8 za dhahabu!

  1. Kuwa fiti, fanya mazoezi
  2. Fuata kanuni bora za afya kwenye lishe
  3. Pima na dhibiti kiwango chako cha sukari ya damu
  4. Pima na dhibiti kiwango chako cha shinikizo la damu presha
  5. Kunywa maji na vimiminika ipasavyo kwako
  6. Epuka kuvufa sigara na matumizi ya tumbaku
  7. Epuka matumizi holela ya madawa ya maumivu
  8. Pima na hakiki ufanyajikazi wa figo zako endapo unaviashiria vya hatari

Contact Us

World Kidney Day
ISN – Global Operations Center
Avenue des Arts 1-2, 6th floor,
1210, Brussels, Belgium
Tel +32 2 808 04 20
info@worldkidneyday.org

Join Our Mailing List

Keep up to date with World Kidney Day news by signing up to receive our emails. We only send about six to eight a year, and promise not to share your details with anyone else. Thanks!